Mwanamume mwenye umri wa miaka 22 kutoka Wisconsin ambaye ghafla alianza kupata kikohozi na kupumua kwa tabu baada ya kupata kifafa na alipo pata nafuu alishtuka kutopata grillz yake ya silver (meno ya bandia) ambayo inasemekana aliimeza bahati mbaya wakati wa kuugua kwake saa chache zilizopita.
Uchunguzi wa kushangaza uliochapishwa hivi majuzi katika Jarida la Kimatibabu la Cureus unasimulia kisa cha mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye, baada ya kupata nafuu kutokana na ugonjwa wa kifafa, alianza kupata kikohozi kikali na kupumua kwa shida na mara moja walifikiria usaidizi wa kimatibabu na uchunguzi wa X-ray ukaonesha kwamba alikuwa na kitu fulani kwenye mapafu upande wa kulia,yaani kwenye njia ya kupitishia hewa kwenye pafu lake.
Kilichoonekana kilikua na urefu wa 4 cm kilionekana kama meno ya bandia, na mwanamume huyo aliwaambia madaktari kwamba alikuwa amevaa grillz yake ya rangi ya gold wakati alipopatwa na kifafa, na hakuweza kuzipata alipopata nafuu.