Basi la Al-Saedy limepinduka alfajiri leo Jumatatu Agosti 7, 2023 katika Wilaya ya Uyui mkoani Tabora huku abiria wakipata majeraha akiwemo mmoja aliyevunjika mkono.
Basi hilo lilikuwa likielekea Dar es salaam kutoka Tabora ambalo liliondoka saa kumi na mbili asubuhi leo.
Diwani wa Kata ya Kigwa, Wilayani Uyui Bakari Kabata amesema ajali hiyo imetokea saa kumi na mbili na nusu kuelekea saa moja katika Kijiji cha Nzigala moja ya vijiji vilivyopo kwenye kata hiyo.
Amesema abiria wamejeruhiwa na mmoja kuvunjika mkono na polisi wamewasili eneo la tukio.
“Ajali imetokea na kujeruhi abiria akiwemo mmoja aliyevunjika mkono na hakuna aliyepoteza maisha,” amesema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao simu yake alipopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa.
Basi hilo na mengine kadhaa yaliondoka mjini Tabora saa kumi na mbili kutoka Stendi Kuu ya Mabasi kwenda mikoa mbalimbali.