Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa, halijapiga marufuku kufanyika mikutano ya nje ya hadhara na ile ya ndani ilimradi inafuata matakwa ya sheria za nchi.
Kilicho pigwa marufuku ni mkusanyiko uliokuwa umeitishwa na Viongozi wa Chadema huko Jijini Mbeya kwa kivuli cha kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani.