
Malkia mpya wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, Zuhura Othman Soud, maarufu kama Zuchu, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kufanya mabadiliko kwenye wasifu wake wa Instagram.
Mwanamuziki huyo nyota ameandika jina “Mrs. Nasibu @diamondplatnumz”, hatua ambayo imetafsiriwa na wengi kuwa ni uthibitisho wa ndoa yake na msanii maarufu Diamond Platnumz.
Hatua hii inakuja siku chache tu baada ya Diamond kutangaza hadharani kuwa yeye na Zuchu wamefunga ndoa, kauli ambayo ilishangaza na kuvutia hisia tofauti kutoka kwa mashabiki.
Kwa muda mrefu, wawili hao wamekuwa wakihusishwa kimapenzi, ingawa mara nyingi wamekuwa wakiepuka kutoa kauli za moja kwa moja kuhusu uhusiano wao.

