Pichani kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. John Nchimbi, akishuhudia Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) – Oganaizesheni, Issa Ussi Haji Gavu akionesha zaidi ya Sh. Mil. 5 zilizochangwa na Wana CCM Pamoja na Wananchi katika Mkutano wa hadhara wa CCM, za kusaidia matengenezo ya gari bovu la Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Antipas Tundu Lisu. Tukio hilo limetokea leo Alhamis Agosti 15, 2024 kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza,wakati Balozi Nchimbi akihitimisha leo ziara yake ya siku mbili jijini humo.Kulia ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa tamati ya Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, amefanya mkutano katika eneo la Furahisha Mkoani Mwanza ambapo amezungumza na Wanachama wa chama hicho tarehe 15 Agosti 2024.
Katika mkutano huo katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla aliongoza wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) zoezi alilo lianzisha lakuweza kumchangia Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tindu Lissu wa Chadema mchango wakufanya matengenezo ya Gari lake.