Klabu ya Singida Black Stars itazindua uwanja wake mpya wa ‘Airtel Stadium’ Machi 24, 2025.
Uwanja huo utazinduliwa kwa mechi ya kirafiki kati ya Singida Black stars dhidi ya Yanga SC.
Kwenye taarifa yao, Singida wamesema kuwa uwanja huo umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa kitovu cha mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa.