Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amejitokeza kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kituo Cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Babati.
Zoezi hilo la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili limeendelea katika Jimbo la Babati mkoani manyara ambapo lilianza tarehe 16/05/2025 na kuhitimishwa leo 22/05 2025.
Akiwa katika kituo hicho cha kujiandikisha Sendiga ametoa wito kwa ambao bado hawajiandikisha kujitokeza muda bado unatosha na Vituo vinafungwa Saa 12:00 Jioni.
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Babati Mjini Edna Moshi amesema zoezi linaendelea vizuri katika Vituo vyote na ameongeza kuwa Wananchi takribani 1294 wamejiandikisha, Wananchi 1599 wameboresha taarifa na Wananchi 498 wamefuta taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Awamu ya Pili.
“Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora”