Joan Martha Mwaipaja, binti wa mwimbaji maarufu wa Injili, Martha Mwaipaja, amewashangaza mashabiki wake baada ya kufunguka wazi kuhusu maombi ya ndoa anayoyapokea kutoka kwa viongozi wa dini. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Joan amesema amekuwa akipokea DM nyingi kutoka kwa wachungaji na manabii mbalimbali wakimuomba mke wao.
Hata hivyo, Joan amesema hana mpango wowote wa kuolewa na mtu mwenye nafasi ya uongozi wa kiroho.
“Sihitaji kuolewa na mchungaji wala prophet, DM zenu msijisumbue. Sihitaji kuwa mama mchungaji wa kanisa. Nitaolewa na mtu wa kawaida hata kama hana umaarufu. Hata kama wewe ni tajiri, sitaki,” ameandika Joan.