Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amesema Iran haipo tayari kwa mazungumzo na Marekani wakati inapewa vitisho na kumtaka Rais Donald Trump ‘kufanya chochote anachoraka’.
“Haikubaliki kwetu kwa wao kutoa amri na vitisho. Siwezi kukaa kuzungumza na wewe. Fanya chochote unachotaka,” Shirika la Habari la Serikali la Iran limemnukuu Pezeshkian.
Kwa upande mwingine, kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollhq Ali Khamenei, Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema Iran haiwezi kulazimishwa kuingia kwenye mazungumzo, muda mfupi baada ya Trump kutuma barua kwa Iran ikiitaka kuingia kwenye mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia.