Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe leo Septemba 08, 2025 amewasili katika Mkoa wa Lindi kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary Jiri.
Akiwa mkoani Lindi, Dkt. Magembe anatarajiwa kushiriki kwenye hafla ya kuhitimu mafunzo kwa wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii katika Mkoa wa Lindi itakayoambatana na makabidhiano ya vishikwambi kwa wahudumu hao wa afya pamoja na kufanya usimamizi shirikishi wa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi na vituo vya afya ngazi ya jamii.