Kufuatia video yake mitandaoni mwanaume huyo ambaye alikuwa akiabudu kwenye kanisa la Dunamis International Gospel Centre, lililopo nchini humo, amesema kuwa kwa miaka mingi, mchungaji wake amekuwa akitumia kitabu cha Mathayo 6:19 kumshawishi kuwekeza katika ufalme wa Mungu.
Mwanaume huyo anadai kwamba amekuwa muumini wa kanisa hilo tangu mwaka 2013, abapo alitoa kitabu chake cha zaka kama thibitisho kwamba amekuwa akilipa kwa miaka mingi.
Mwanaume huyo ameongeza kuwa kutokana na hali ya ukata inayomkabili, amesema hataki njaa imtafune hapa duniani na kusisitiza kanisa hilo limrudishie zaka zake ili pia aweze kuwalipa wafanyakazi wake.