MWANAMUZIKI mwenye ushawishi wa Ghana ambaye pia ni maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii Mona Faiz Montrage, al maarufu Hajia4Real, amesafirishwa hadi nchini Marekani kushitakiwa katika utapeli wa kimapenzi wa dola milioni 2 ($1.6m)
Biashara ya uhalifu anayodaiwa kuhusishwa nayo inasemekana kuwalenga wanaume wa Kimarekani wenye upweke pamoja na wanawake na wakati mmoja kujifanya kuwa ameolewa na mmoja wa waathiriwa ili kuendeleza utapeli wake.scheme.
Shirika la ujasusi la Marekani (FBI) katika taarifa yake lilionyesha kuwa ameshitakiwa kwa mashitaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kutekeleza wizi na utakatishaji wa pesa.
Anaweza kupewa hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela kwa kila kosa iwapo atapatikana na hatia.
Alishitakiwa kwa kusaidia katika kupokeana kutoa hundi za pesa zilizoibiwa, uhalifu unaoweza kumfunga jela kwa miaka mitano na kumi.
Mona mwenye umri wa miaka 30, alikamatwa tarehe 10 Novemba mwaka jana nchini Uingereza na kusafirishwa hadi Marekani Ijumaa.
Alikana mashitaka yote alipofikishwa mahakamani mbele ya majaji Jumatatu.
Maafisa wa Marekani wameelezea hofu yao kuhusu ulaghai wa kimapenzi unaowalenga wazee binafsi na kuelezea haja ya kuwawajibisha wahusika.
Montrage anadaiwa kuwa sehemu ya mtandao wa uhalifu katika Afrika magharibi, wakiwemo matapeli wa kimapenzi nchini Marekani kati ya mwaka 2013 na 2019.