Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano wa Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesimama bungeni kufafanua kuhusu kufungwa kwa baadhi ya nyumba za starehe nchini kufuatia muongoza wa mbunge wa Geita Joseph Musukuma ambaye alitaka kujua hatima ya Bar zilizofungwa
Waziri Jafo amesema.. “Maelekezo kwa mujibu wa sheria ni kwamba kila eneo lina utaratubu wake wa kuendesha biashara katika eneo hilo kama Night Club watu wanaweza kupiga muziki kwa kadiri wanavyohitaji hawawezi kuathiri watu wengine lakini kwenye maeneo ya Bar kuna utaratibu wake ndio maana hivi karibuni katika utekelezaji wa sheria hiyo taasis ya Nemc kwa kushirikiana na serikali za mitaa waliwafuatia watu waliokiuka sheria na Bar takribani 89 zilisimamishwa na asubuhi yake nilitoa muongozo”-Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingora Dkt. Selemani Jafo