Halmashauri za miji 45 hapa nchini zinatarajiwa kunufaika na Ujenzi wa miradi ya uboreshaji wa miundombinu ya miji yenye thamani ya Dola milioni 410 katika maeneo ya barabara, Vituo vya Mabasi pamoja na mitaro ambapo Ujenzi wake utaanza mwezi July mwaka huu.
Akizungumza na wana habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi ya zabuni kutoka kwenye miji inayotekeleza miradi hiyo, Mratibu Msaidizi wa Mradi huo kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na TARURA Mhandisi Emmanuel Manyanga alisema kuwa mradi huo unakwenda kutatua changamoto za kimiundombinu na kuboresha miji.
Mradi huo ambao ambao unafadhiliwa na serikali ikiwa ni mkopo kutoka bank ya dunia wenye mashariti nafuu unaratibiwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kupitia wakala wa barabara za Vijijini na Mijini Tarura ambao wamepewa mamlaka ya kusimamia mradi huo ambao unatekelezwa kwa miji arobaini na tano ambayo imeganywa kwa awamu tatu ambapo kundi la kwanza litakaloanza mradi huo ni kundi la kwanza la miji kumi na mbili, huku ndio la pili likiwa na kundi la miji kumi na tano na kundi la tatu ni kundi la miji kumi na nane.
Aidha amesema kuwa makubaliano ya Serikali pamoja na bank ya dunia ni kutekeleza miradi yote ya miji 45 kwa gharama ya dola za kimarekani 410 bila kodi ya ongezeko la dhamani yaani VAT ambapo amesema kuwa katika utekelezaji bank ya dunia imeridhia kuanza kutoa Jumla ya dola 278 fedha mbazo zitatoka kwaajili ya kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza.
“kwakweli tunashukuru sana Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluh Hassan na Waziri wetu wa Tamisemi pamoja na mtendaji mkuu wa Tarura kwa usimamizi mzuri wa miradi hii mpaka hapa tulipofikia katika hatua ya kuanza utekelezaji” Alisema Manyanga
Kwa Upande wao Wajumbe wa bodi ya zabuni katika ngazi za Halmashauri wamesema kuwa mradi huo utakwenda kuboresha baadhi ya maeneo ya miji na kukuza Uchumi wa maneo hayo.
Mradi huo wa kuboresha Halmashauri za Mji inakwenda Sambamba na kuzijengea uwezo Halmashuri katika kukusanya mapato ikiwemo huduma mbalimbali kama kupima Ardhi na uendeshaji wa mifumo ya Mapato kwa Ufanisi.