Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasili Dar es salaam na amepokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Albert Chalamila na viongozi wa Mkoa huo kushiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni 2023.
Mkutano huo wa TNBC utaongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.