Rais wa Urusi Vladimir Putin mapema siku ya ijumaa alimshukuru rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu kwa juhudi zake za kuwakomboa wafungwa wa vita nchini Ukraine na kupongeza kile alichosema ni kupanua uhusiano wa kiuchumi kati ya Moscow na Abu Dhabi.
Naye rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) alimwambia Rais wa Urusi Vladimir Putin kwamba taifa lake lingependa kuimarisha uhusiano kando ya kongamano la kiuchumi nchini Urusi.
“Nimefurahi kuwa hapa leo na wewe, na tunataka kuendeleza uhusiano huu, na tunaweka imani yetu kwako kufanya hivyo,” Sheikh Mohammed alimwambia Putin.
Jimbo hilo la Ghuba halijajiunga na nchi za Magharibi katika kuiwekea vikwazo Moscow na limeshikilia kile inachosema ni msimamo wa kutoegemea upande wowote katika vita vya Ukraine.
“UAE inaendelea kuunga mkono juhudi zote zinazolenga kufikia suluhu la kisiasa kwa njia ya mazungumzo na diplomasia – kuelekea amani na utulivu duniani,” Sheikh Mohammed alitweet baada ya mkutano huo.