Na Nyamiti Alphonce
Kamati ya ulinzi na usalama kushilikiana na Ofisi ya Madini Kahama wameanza mikakati ya kudhibiti utoroshaji wa madini ili serikali iweze kunufaika na mapato yanayotokana Biashara hiyo.
Kupitia ziara ya kukagua masoko ya dhahabu, migodi midogo na kuongea na Wachimbaji na wanunuzi wa bidhaa hiyo mkuu wa wilaya hiyo Mh. Mboni Mhita amewataka kutojihusiha na vitendo vya utoroshaji wa madini kwani sheria kali zitachukuliwa kwaatakaye bainika kujihusisha na udaganyifu wa Aina yoyote.
Sambamba na hayo Amesema serikali Wilayani humo itakwenda kuboresha maeneo ya masoko ikiwemo kujenga uzio utakaofanya wanunuzi na wauzaji kutumia milango maalumu ya kuingilia na kutoka kuepusha udaganyifu
Hata hivyo Akamtaka mkuu wa kituo cha polisi Kahama Kuongeza ulinzi kwenye maeneo ya uzalishaji na uuzaji wa madini kuweza kubaini udaganyifu
Kwaupande wake Afisa madini wilaya ya Kahama Bw. Germia Hango Amesema kupitia Ofisi ya Madini Kahama kwa kushirikiana na jeshi la polisi wameendelea kuhakikisha wanadhibiti utoroshaji wa madini kwa kiasi kikubwa.
Baadhi ya wafanyabiashara wa dhahabu mjini humo wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji na makota namna nzuri ya uuzaji na ununuzi wa madini hayo.