Na Bukuru Daniel – Burundi
Wafanya biashara katika soko la Ruvumera mjini Bujumbura wamekataa kufungua maduka wakiishinikiza serikali kupunguza kodi baada ya kupandiswa na mamlaka ya mapato OBR.Wanasema kodi hiyo siyo rafiki katika shughuli zao na watafanya kazi kwa hasara.