Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyokutana katika kikao chake maalumu tarehe 1 Oktoba, 2023, jijini Dar es Salaam, imefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa Jumuiya za Umoja wa Wanawake (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).
Katika kikao hicho, Kamati Kuu kimemteua Ndugu Jokate Mwegelo, kuwa Katibu Mkuu wa UWT, kabla ya uteuzi huo Ndugu Mwegelo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.