Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametangaza ongezeko la Dola 32 za Marekani (Takriban Tshs. 80,320) kwa wenye mshahara wa kima cha chini kwa muda wa miezi 6 wakatia ambao wafanyakazi nchini humo wakijiandaa kuanza mgomo usio na kikomo kuanzia Oktoba 3, 2023.
Ongezeko hilo linapelekea mshahara wa kima cha chini wa kila mwezi kuwa Dola 70 (Tshs. 175,700), huku vyama vya wafanyakazi vikitaka uongezwe hadi Tshs. 640,050 ili kukabiliana na ongezeko kubwa la gharama za maisha tangu Rais Tinubu aondoe ruzuku ya mafuta.