Katika dakika chache zilizopita, tumesikia kutoka kwa msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la White House, John Kirby.
Kirby anasema serikali ya Marekani haina nia ya kupeleka wanajeshi Israel, lakini italinda maslahi ya Marekani katika eneo hilo.
Anasema maombi zaidi ya usalama yanatarajiwa kutoka Israel, ambayo Marekani itajaribu kutimiza haraka iwezekanavyo.
Kirby pia anasema “hakuna swali kwamba kuna kiwango fulani cha ushirikiano” na Iran katika kuunga mkono Hamas, Marekani haijaona ushahidi kwamba Iran ilihusika moja kwa moja.
Ripoti katika gazeti la Wall Street Journal inadai kuwa Iran ilishiriki katika kusaidia Hamas kujiandaa kwa shambulio hilo la kushtukiza.