Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa taarifa ya mwenendo wa Sekta ya Mawasiliano katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba, 2023 na kueleza kuwa kumekuwa na ongezeko la Watumiaji wa Intaneti kwa 1.24% kutoka Watumiaji 34,047,407, mwezi Juni 2023 hadi kufikia 34,469,022 mwezi Septemba 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA , Dkt Jabir Bakari ametoa taarifa hiyo Oktoba 25, 2023 jijini Arusha ambapo amesema baadhi ya sababu kuu zinazochangia ongezeko la matumizi ya intaneti zimeendelea kuwa ni uwepo wa maudhui ya Kiswahili kwenye mtandao ikijumuisha kuongezeka kwa programu-tumizi (applications) kwa lugha ya Kiswahili.