Wakati mitihani ya kitado ya taifa kwa Kidato cha pili na ile ya Kidato cha nne ikitarajia kuanza kufanyika kuanzia mwezi Novemba mwaka huu Walimu na wanafunzi wametakiwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa mitihani ili kuondoa hatari ya kufutiwa mitahani na shule kufungwa kwani wizi wa mitihani haukubaliki popote hapa nchini.
Akizungumza Katika mahafali ya 16 ya Shule ya sekondari Mgeni Rasmi Marco Kabadi ambaye ni Diwani wa kata ya Kisesa iliyopo Magu mkoani Mwanza amesema ” Kuelekea Mitihani ya Kidato cha pili na ile ya Kidato cha nne tunawaomba wanafunzi pamoja na waalimu wajiandae ipasavyo kuhakikisha mitihani inafanyika kwa ufanisi jambo litakaloondoa Udanganyifu wa mitihani kwa wanafunzi hao”
Sambamba na mahafali hayo kufanyika Diwani wa Kata ya Kisesa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Marco Kabadi akimwakilisha mgeni rasmi kwenye mahafari ya 16 ya shule ya sekondari Pasiansi ambaye ni Mkurugenzi wa Qwihaya General ambaye ni Mnec Leonard Qwihaya ameahidi kuchangia zaidi ya Shilingi Milioni tatu kwa ajili ya ununuzi wa vitanda 20 na viti vya walimu 30 lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi kwenye ufaulu kwa wanafunzi pamoja na utendaji kazi kwa waalimu ambao wamekuwa wakikosa viti bora vya kukaa wawapo ofisini.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pasiansi Mtaki Shanyangi amesema maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne yanaendelea vizuri kwa kushirikiana na wazazi viongozi wa mitaa na kata huku akiahidi kudhibiti mianya yote ya udanganyifu wa mitihani kwa kuwaandaa vyema wanafunzi,