Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Agosti 27, 2024 amewasili NairobiĀ kuhudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwa ni mualiko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Dkt. William Samoei Ruto. Hafla hiyo itafanyika katika Ikulu ya Nairobi na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi mbalimbali, tarehe 27 Agosti, 2024.