Rais Paul Biya wa Cameroon, mwenye umri wa miaka 92, ametangaza rasmi kuwa atawania tena urais kwa mara ya nane katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu. Tangazo hilo limekuja kupitia ukurasa wake wa X, akisema kuwa bado ana dhamira ya kulitumikia taifa.
Biya ameiongoza Cameroon tangu mwaka 1982, na hajawahi kushindwa uchaguzi wowote. Mwaka 2008 alifuta kikomo cha mihula ya urais, jambo lililomruhusu kuendelea kugombea. Katika uchaguzi wa 2018, alitangazwa mshindi kwa zaidi ya asilimia 71 ya kura, ingawa upinzani ulilalamikia kasoro kubwa katika mchakato huo.
Iwapo atashinda tena, Paul Biya ataendelea kushikilia rekodi kama rais mzee zaidi duniani akiwa madarakani, na anaweza kuendelea kuongoza hadi karibu na umri wa miaka 100.