
Akizungumza wakati wa kukabidhi mchango huo Oktoba 28,2026 kwa niaba ya Jeshi la Polisi wilayani humo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP. Janeth Magomi, amewapongeza wananchi wa Maganzo kwa juhudi zao za kuimarisha ulinzi na usalama huku akiahdisi kutoa matofali 1,000 na akiwataka kuendelea kudumisha amani na utulivu, hususan katika kipindi cha mwisho wa mwaka.
Aidha, ameendeleza kampeni ya *Ongea na Kamanda*, akiwahimiza wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na viashiria vyake kwa Jeshi la Polisi, pamoja na kutunza miundombinu ya Serikali na kushirikiana katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
Katika hatua nyingine, Kamanda Magomi alikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Sungusungu katika kata hiyo na kuahidi kuchangia matofali 1,000 ili kusaidia kukamilika kwa mradi huo hukuakikubali ombi la viongozi wa Sungusungu la kuwa msimamizi wa jengo hilo, hatua inayolenga kuunga mkono juhudi za jamii katika kuimarisha shughuli za ulinzi shirikishi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kishapu, SP Ester Gesogwe, amesema Sungusungu ni kundi muhimu linaloshirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi katika kuzuia na kudhibiti uhalifu, hivyo mchango huo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya usalama.
“Ninawasihi wananchi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa Kata ya Maganzo na kukuza uchumi wa kaya na uchumi jumuishi unaowanufaisha wananchi wote,” amesema Tandiko.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi huo, Kamanda Mkuu Mwanamke wa Sungusungu Kata ya Maganzo, Tayaya Rashidi, amesema eneo la ujenzi limetolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata hiyo hivyo jengo hilo litakuwa na vyumba viwili vya ofisi, ukumbi wa mikutano na matundu nane ya vyoo, likiwa na makadirio ya gharama ya Shilingi milioni 33.5.
Amesema lengo la ujenzi huo ni kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kupitia ushirikiano wa Sungusungu na Jeshi la Polisi, pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wananchi kuwasilisha shida, malalamiko na taarifa zao katika ofisi maalumu.
Kupitia hafla hiyo Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Maganzo ameahidi kuwa yeye na wafanyabiashara hao watachangia mifuko mitano ya saruji na Sadick Mohamed afisa usafirishaji wa taka za sokoni akiahidi kutoa Tsh. 100, 000.
