
Na Nyamiti A, Nyamiti
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, Amekabidhi mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.167 kwa vikundi 96 vya wajasiriamali Manispaa ya Kahama.
Fedha hizo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, zimegawanywa kwa makundi matatu – vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Mhita amewaonya wanufaika kutochanganya mikopo na anasa na badala yake wafanyie Miradi waliyokusudia na kurejesha fedha hizo ili wengine waweze kunufaika.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, amesema katika kipindi hiki Manispaa imetoa,Bilioni 1.428 kwa vikundi 45 vya vijana,Milioni 708.52 kwa vikundi 46 vya wanawake, Milioni 31 kwa vikundi 5 vya watu wenye ulemavu
Kibetu amesema Tangu 2025 hadi sasa, jumla ya Shilingi Bilioni 6.377 zimetolewa kwa vikundi 335.
Mstahiki Meya Kaniki Mataluma amesema kwa mwaka wa fedha ujao, Manispaa inalenga kutoa zaidi ya Bilioni 4.
Milaji Mrasi, mjasiriamali mwenye ulemavu aliyepata mkopo, amesema utaratibu wa sasa wa kila mtu kupata mkopo mmoja mmoja ni bora kuliko ule wa zamani wa vikundi kwa walemavu.
