
Kampuni ya Lanxi Yema nchini China inafanyia majaribio helmeti maalumu za waendesha pikipiki zenye teknolojia ya Airbag, inayowezesha mifuko ya hewa kufunguka kwa haraka wakati wa ajali.
Teknolojia hiyo imeundwa kusaidia kupunguza madhara yanayoweza kutokea kwa kulinda kichwa na shingo ya mwendesha pikipiki wakati wa ajali.
Ubunifu huo umevutia hisia za watu baada ya video za majaribio yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, huku ukitajwa kuwa sehemu ya juhudi za kuboresha usalama wa waendesha pikipiki.
