Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika leo Jumatano Oktoba 4, 2023 huku bei ya dizeli ikizidi kupaa ikilinganishwa na mwezi Septemba.
Kwa mwezi huu bei za rejareja za mafuta katika
mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama ifuatavyo;
Dar es Salaam lita ya petroli ni Sh3,281, dizeli Sh3,448 na mafuta ya taa yakiuzwa Sh2,943. Tanga lita ya petroli ikiuzwa Sh3,327, dizeli Sh3,494 na mafuta taa Sh2,989.
Mkoa wa dizeli imezidi kupaa mara dufu ikiuzwa kwa lita Sh3,520, petrol Sh3,353 na mafuta ya taa Sh3,016.
Ewura imetaja sababu ya mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Oktoba 2023 ikiwa ni kupanda kwa gharama za bidhaa hiyo katika soko la dunia kwa hadi kufikia asilimia 4.21 na gharama za uagizaji kufikia asilimia 17 kwa petroli, asilimia 62 kwa dizeli na asilimia 4 kwa mafuta ya taa.
Pia, uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta
duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa na mataifa ya magharibi.