JUMLA ya majina saba pekee kati ya 12 ya wachezaji wa kigeni ndiyo yametangazwa kubakishwa katika msimu ujao huku wengine wakipewa ‘thank you’ akiwemo Lionel Ateba..
Chanzo kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, tayari wachezaji wanaowaacha wamewapa taarifa za kuachana nao na ruksa kwenda kutafuta changamoto mpya kwingine.
Wachezaji hao wa kigeni waliobakishwa ni Steven Mukwala, Jean Ahoua, Elie Mpanzu, Chamou Karaboue, Joshua Mutale, Moussa Camara na Valentino Nouma.