
Mwimbaji wa Bongofleva kutokea Khan Music, Mbosso amesema baada ya miaka minane, ndipo kafanikiwa kuonana na mwanamuziki mwenzake Aslay.
Mbosso amefunguka hayo kupitia Instagram ambapo ameposti picha zake na Aslay walizopiga baada ya kukutana uwanja wa ndege.
“Imagine mara ya mwisho tumekutana ni mwaka 2017 na tumekuwa tukiwasiliana bila kuonana.” ameandika Mbosso na kuongeza.
“Baada ya miaka takribani nane, jana ndio tumekutana tena na kwa bahati mbaya tu kila mtu akiwa kwenye mihangaiko yake yakwenda kutafuta rizki. Was nice to See you my legendary brother Aslay.” amesema Mbosso.
Utakumbuka Aslay na Mbosso walikuwa miongoni mwa wasanii wanne waliounda kundi la Yamoto Band. Wengine ni Enock Bella na Beka Flavour.
