Mwimbaji na Mtunzi wa nyimbo za Injili @sarah_ndosi Jumapili ya tarehe 29 Januari 2023 amezindua Album inayokwenda kwa jina la JAWA.
Uzinduzi huo umefanyika katika kanisa la Calvary Temple ambapo album hiyo iliwekwa wakfu na Mchungaji wa Kanisa Hilo Pastor Phillip David.
Sarah amesema sehemu ya mapato atakayoyapata atapeleka katika makundi ya watoto ili waweze kuendelea na masomo.
Na kupitia ukurasa wake wa instagram @sarah_ndosi amemshukuru Mume wake kipenzi kwa kumshika mkono katika mchakato mzima wa uzinduzi wa albamu hiyo:
“Shukurani nyingi sana kwa mume wangu kwa kazi nzuri ya branding aliyofanya kwenye album ya JAWA kupitia kampuni yetu ya graphics design na branding @orikah.ent Na hata sasa tunapokea wanafunzi wanaotaka kujifunza Graphics design na branding pamoja na kazi za branding.” aliandika
Kwasasa album ya JAWA inapatikana kwa njia ya digital platforms zote pia unaweza ipata kwa njia ya Flash.
Kwa maelekezo zaidi na jinsi ya kuipata albamu hii mpigie simu Sarah Ndosi kupitia simu namba +255757531093 au tembelea @sarah_ndosi kwa maelezo na maelekezo zaidi ya jinsi ya kuipata.