Beyonce amevunja rekodi hiyo kwa kuwa na tuzo 32 baada ya kutwaa tuzo nne kati ya tisa alizochaguliwa kushiriki akishinda wimbo bora wa R&B, densi bora/rekodi ya kielektroniki, albamu bora ya densi/kielektroniki na utumbuizaji bora wa kitamaduni wa R&B.
Msanii huyo amefikia rekodi hiyo ambayo ilikuepo muda mrefu tangu 1998 ilikua ikishikiliwa na mtayarishaji wa muziki Georg Solti mwenye Grammy 31 katika sherehe ya 65 ya tuzo za Grammy, zilizofanyika katika ukumbi wa Crypto.com huko Los Angeles nchini Marekani, jumapili usiku Februari 5, 2023.
Solti anatambulika kama mtayarishaji wa muziki ambapo kwa umakini wa uundaji wa muziki wake.
Wasanii wengine waliotikisa kwenye tuzo hizo ni Kendrick Lamar Duckworth aliyetwa tuzo ya albamu bora ya Rap, akitamba na albamu ya ‘Mr Morale and the Big Steppers.’
Wakati huo wanamuziki Sam Smith na Kim Petras wameshinda tuzo ya kikundi bora cha nyimbo za pop, wakitamba na ngoma yao ya ‘Unholy’, naye Samara Joy ameshinda tuzo ya msanii bora mpya kwa mwaka 2023.
Katika tukio hilo, mke wa Rais wa Marekani, Jill Biden alitoa tuzo kwa wimbo uliosababisha mabadiliko uliokuwa ukitumika kwenye maandamano nchini Iran.