Kijana Philimon Shukrani (19) mkazi wa mtaa wa Mnubi, Kata ya Kwangwa Manispaa ya Musoma mkoani Mara amekutwa amejinyonga ndani baada ya wazazi wake kuondoka na kwenda msibani Ukerewe huku chanzo cha kujinyonga kikisadikiwa kuwa ni kuachwa kwenda kumzika bibi yake wilayani Ukerewe.
Wakizungumzia namna ambavyo waliweza kugundua kutoweka kwa kijana hiyo baadhi ya majirani wanasema, “sisi hatukumuona kwa siku nzima ya Jumamosi tukashikwa na wasiwasi kwani taa za nyumbani kwao zilikuwa zinawaka muda wote na pia haikuwa kawaida yake kutokufanya kazi ya kufagia uwanja,” amesema Tano Maige balozi wa Mtaa wa Kiara B.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo amesema, “Mnamo majira ya saa 5:00 siku ya Jumamosi lilipigiwa simu na wananchi wangu wakiniambia kuna kijana amejinyonga ndani ya nyumba na wazazi wake hawapo niliweza kufika katika eneo la tukio na kukuta kweli milango imefungwa lakini kwa kuegeshwa na tulipoingia ndani tulikuta amejinyonga sebuleni” amesema Maximilian Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa.