Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayay amesema Klabu za Simba na Yanga bado zina nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano ya kimataifa endapo watapata ushindi kwenye michezo yote ambayo watacheza katika Uwanja wao wa nyumbani.
Mayai amesema hayo Jumatatu ya Leo Februari 13, 2023 kufatia klabu vya Simba na Yanga kupata matokeo mabovu, Simba ikifungwa 1-0 na Horoya AC ya Guinea kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika pamoja na Yanga kufungwa 2-0 Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir ya Tunisia.
”Iwapo wakacheza vyema katika uwanja wa nyumbani mimi naamini zitakwenda katika hatua inayofata” Mayai
Kwa upande mwingine:Wachezaji wakongwe wa zamani wa Simba na Yanga, Dua Saidi wa Simba na Juma Pondamali wa Yanga wametoa ushauri kwa mabenchi ya ufundi kuzingatia maumbile ya wachezaji pindi wanavyopanga vikosi vyao kwenye michezo hii ya Kimataifa
Wawakilishi hao watanzania wanatarajiwa kuwasili nchini kuanzia Jumanne ya kesho Februari 15, 2023 kwa timu zote kuingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo ijayo ambapo Simba itawakaribisha Raja Casablanca ya Morocco na Yanga itacheza na TP Mazembe ya DR Congo wikiendei hii.