Rais Samia Suluhu ametangaza kununua kwa Sh5 milioni kila bao litakalofungwa na Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa ya mwisho wa wiki hii.
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema hayo leo huku timu hizo zikiwa na kibarua kwa mechi ya pili hatua ya makundi baada za kwanza kufungwa ugenini.
Simba itacheza Jumamosi dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika saa 1:00 usiku uwanja wa Mkapa na Yanga itaikaribisha TP Mazembe Jumapili saa 1:00 usiku katika mechi ya Kombe la Shirikisho.