Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kimbunga cha kitropiki kukumba pwani ya mashariki ya Madagascar, huku mvua kubwa ikiambatana na upepo mkali kuangusha mapaa ya nyumba na kusababisha dhoruba kali.
Ofisi ya Kitaifa ya kudhibiti majanga ilisema mwanaume mwenye umri wa miaka 27 alizama kwenye bandari ya Mahanoro, Mashariki mwa Madagascar.
Kimbunga Freddy kimetua Jumanne, wiki kadhaa baada ya dhoruba lingine la kitropiki kuua watu 33 na kuwaacha maelfu bila makazi.
Mawimbi yake ya dhoruba yalipasua nyumba na uwanja wa michezo wa Maranjary.
Maelfu ya watu wamehamishwa kutoka Mkoa wa Vatovavy, wa kwanza kupigwa.
Shule na usafiri umesitishwa katika maeneo kando ya njia yake katika mikoa 10 katika taifa la kisiwa hicho.
Mvua kubwa, upepo mkali sana, bahari iliyochafuka na mafuriko ya pwani yanatarajiwa kuendelea katika maeneo ya athari.
Vimbunga vya kitropiki hupoteza nguvu zao vinaposogea nchi kavu. Utabiri wa hali ya hewa unatabiri kuwa kimbunga Freddy atadhoofika kwa dhoruba kali ya kitropiki kitapoelekea Msumbiji, Jumatano.
Hapo awali, kimbunga Freddy kilisababisha uharibifu fulani huko Mauritius, na kusababisha mafuriko katika hoteli za ufuo.
Hata hivyo, nchi ya kisiwa cha Bahari ya Hindi iko katika hatari kubwa ya vimbunga.
Hukumbwa na wastani wa vimbunga 1.5 kila mwaka, kiwango cha juu zaidi barani Afrika, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu.
Kimbunga hicho kilidhoofika kidogo mara kilipotua Madagascar, iliyo karibu na pwani ya kusini-mashariki mwa Afrika, kikiwa na upepo mkali unaozidi 130km/h (81mph).
Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini ilionya kuwa mvua kubwa itaendelea kunyesha katika njia yake.
“Bahari inaendelea kuchafuka… na hatari kubwa ya mafuriko katika pwani itaendelea usiku mmoja,” ilisema.
Maafisa pia walisema watu 7,000 walikuwa wamehamishwa kwa urahisi kutoka eneo la pwani moja kwa moja kwenye njia ya kimbunga Freddy na mawimbi ya maonyo yanaweza kufikia zaidi ya 8m (26ft) yalitolewa na Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu.
Baadhi ya watu walitumia mifuko ya mchanga kukinga paa zao kama tahadhari.
“Milango na madirisha yote yalianza kutikisika,” alisema Tahina, mkazi wa Mananjary, mji wa pwani wenye takriban watu 25,000 kilomita 30 kutoka mahali ambapo kimbunga kilitokea mara ya kwanza.