Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu watano waliokuwa wanajifanya waganga wa kienyeji kwa tuhuma za mauaji ya mwalimu Monica Patrick (31) mkazi wa Itilima mkoani Simuyu baada ya kumuibia fedha shilingi milioni 9.5 na kisha kumnyonga.
Imeelezwa marehemu alifika mkoani mara kwa madai ya kumfanyiwa maombi ya kumsaidia katika biashara yake ya madini.
Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoani humo amesema kuwa baada ya watuhumiwa hao kufanya mauaji hayo walitumia simu ya marehemu kuwasiliana na Dada wa marehemu na moja ya wafanyakazi wenzie.
Kamanda Tibishibwamu amesema kuwa walipo wafanyia mahojiano watuhumiwa hao imeonekana wamekuwa wakifanya mauaji hayo kwa muda mrefu na mpaka sasa wameisha fanya mauaji kwa zaidi ya watu 20.