Waendesha mashtaka wa Ufaransa Jumatatu walifungua uchunguzi kuhusu madai ya ubakaji na beki wa pembeni wa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi!
Mwanamke mwenye umri wa miaka 24 amemshutumu mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco kwa kumbaka nyumbani kwake katika kitongoji cha Paris mnamo Februari 25.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikithibitisha makala katika gazeti la Parisien, mwanamke huyo aliripoti tukio hilo katika kituo cha polisi siku ya Jumapili lakini hakufungua mashtaka.
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma inayoshughulikia kesi hiyo huko Nanterre ilikataa kutoa maoni yake, lakini ililalamikia kwamba
“taarifa ambazo tayari zimetolewa kwa umma kwenye vyombo vya habari zilidhoofisha uchunguzi muhimu ili kujua ukweli”.
Hakimi alikuwa sehemu ya timu ya Morocco iliyomaliza katika nafasi ya nne katika Kombe la Dunia
Na Jumatatu jioni alikuwa kwenye hafla ya tuzo za FIFA huko Paris, ambapo alichaguliwa na kutajwa kama “FIFPro men’s world team of the year”