Habari mbaya zilizotufikia hivi punde leo Mei 12, 2023 zinaeleza kuwa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Kamilius Membe, amefariki dunia muda mfupi uliopita.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa watoto wake ameeleza kuwa ni kweli kiongozi huyo ameaga dunia katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa, taratibu za msiba zinafanyika nyumbani kwa mwanasiasa huyo mkongwe maeneo ya Mikocheni jijini Dar.
Kwa mujibu wa mtoto huyo, baba yake amepata changamoto ya kifua na kupelekwa hospitalini hapo alfajiri ya leo ambapo amepoteza maisha muda wa saa 3:00 asubuhi.