Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete ameongoza uzinduzi wa harambee ya kampeni ya GGML Kili Challenge yenye lengo la kukusanya Sh bilioni 2.3 kwa ajili ya mapambano dhidi VVU na Ukimwi ambapo katika harambee ya uzinduzi Jumla ya Dola za Marekani 700,000 (sawa na Sh bilioni 1.6) zimepatikana.
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete ameongoza uzinduzi wa harambee ya kampeni ya GGML Kili Challenge yenye lengo la kukusanya Sh bilioni 2.3 kwa ajili ya mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi ambapo katika harambee ya uzinduzi Jumla ya Dola za Marekani 700,000 (sawa na Sh bilioni 1.6) zimepatikana
Kampeni hiyo iliyoasisiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ilianzishwa mwaka 2002 na kufikia makundi mbalimbali yaliyo katika maeneo hatarishi kwenye janga hilo.
Akizunguma katika harambee hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Dk. Kikwete aliipongeza GGML na TACAIDS kwa ushirikiano walioufanya na kuanzisha kampeni hiyo inayounga mkono jitihada za Serikali kudhibiti maambukizi ya VVU/ UKIMWI.
“Endeleeni kuitangaza GGM Kili Challenge kwa kupitia mabalozi mbalimbali na celebrity (watu maarufu) ili kampeni hii iwe jambo linalozungumzwa duniani,” alisema.
Tanzania bila UKIMWI, inawezekana! Msemo huo ulikuwa wa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong mbali na kuishukuru Serikali kwa kuunga mkono kampeni ya GGML Kili Challenge alisema wakiwa wadau wa mapambano hayo ya UKIMWI na VVU, GGML imepokea msaada ambao uliiwezesha Kili Challenge kupiga hatua kubwa hadi kufikia kuwa mfuko wa kimataifa, wenye kushirikisha wapanda mlima na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.
Kwa upande wake Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo amesema tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo makundi mbalimbali yamefaidika ikiwa kuazishwa kwa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu – Moyo wa Huruma kilichopo Geita.