Mwanamke mmoja anang’aa kwa furaha hatimaye kufunga ndoa na barafu wa moyo wake baada ya kusubiri kwa miaka na mikaka.
Licha ya umri wake, mwanamke huyo mrembo alijawa na raha moyoni baada ya kuwa mke kwa mara ya kwanza. Alimshukuru Mungu kwa kumkumbuka na kumpa mume mtanashati.
Akishiriki ushuhuda wake na mumewe, mwanamke huyo mwenye furaha kutoka Ghana alisema alikutana na mume wake miongo mitatu iliyopita.
“Tulikutana takribani miaka 30 iliyopita, lakini nilikuwa nimemsahau miaka ilipopita. Tulikutana kwa mara nyingine tena wakati wa kipindi cha maombi wakati Mungu alipoweka sawa hatima yetu. Matendo ya Mungu hayawezi kuelezewa. Yote haya ni Mungu tu. Sifa na utukufu wote ni wake,” mwanamke huyo mwenye furaha alimwambia Millicent Abraham.
Pia aliwatia moyo wanaume na wanawake wasimwache Mungu kwani baraka zitawajia wakati wake ukifika.
Wenzi hao walifanya harusi ya kukata na shoka kanisani ili kuhitimisha mapenzi yao na kubadilishana viapo mbele ya wageni.
Mwanamke huyo alisema harusi yao ilifadhiliwa kimiujiza, ikiwa ni pamoja na gauni na mavazi ya mume.
Ilikuwa harusi nzuri iliyowaacha wengi katika mshangao huku wachumba hao waliokuwa na pengo la umri wa miaka 10 kati yao wakifunga ndoa.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 63 alisema alihisi kama “kusakata densi” baada ya kujishindia mke mrembo.
Watu katika mitandao ya jamii waliwafurahia wanandoa hao na waliwatumia jumbe za kuwapongeza huku wakikubaliana nao kwamba Mungu ni muweza yote.