Baada ya klabu ya Azam kumsajili kiungo Feisal Salum kutoka Young Africans SC kwa mkataba wa miaka mitatu, atavaa jezi namna 6 ndani ya klabu yake hiyo mpya.
Baada ya kumalizika kwa sakata lake la mgogoro wa muda mrefu wa kimkataba na klabu ya Yanga, Feitoto amesema ana furaha kubwa sakata hilo kumalizwa na amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia kumaliza mgogoro huo.
“Namshukuru Rais kwa kulimaliza hili jambo, nitazidi kumuombea katika majukumu yake.
“Nawashukuru pia mashabiki wa Yanga na Viongozi kwa upendo walionionesha,” amesema Feitoto muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Azam hadi 2026.