Baada ya baadhi ya wajumbe wa Kamati tendaji ya Chama Cha Walimu Tanzania CWT kuandamana na hadi makao Makuu ya ofisi hizo jijini Dodoma na kutaka kusitisha shughuli za kiofisi za katibu mkuu wa chama hicho Josephat Maganga kwa madai ya matumizi mabaya ya Ofisi.
“Zipo mamlaka ambazo zimewekwa na chama kwa mujibu wa katiba na zimepewa mamlaka ya kuchua hatua kamati ya utendaji taifa haina mamlaka hata kidogo ya kumwajibisha kiogozi yoyote aliyechaguliwa na mkutano mkuu wa taifa kwa mujibu wa katiba ya chama cha walimu Tanzania mamlaka yenye uwezo wa kumsimamisha kiongozi aliyechaguliwa na mkutano mkuu kama anatatizo ni baraza kuu la Taifa na lenye uwezo kabisa ni mkutano mkuu wa Taifa”
Hata hivyo madai yaliyotolewa na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Thobias Sanga mjumbe wa kamati tendaji Taifa amesema kikao hicho kilibaini kukiukwa kwa katiba na kanuni za chama hicho hivyo wameamua kuazimia kusimamisha shughuli za kila siku katibu mkuu jambo ambalo limetajwa kuwa ni kinyume cha kifungu 21.3(a,b na c) cha katiba ya chama cha walimu hivyo kamati imengilia majukumu ya baraza kuu na mkutano mkuu wa Taifa wa chama hicho.
Hata hivyo katika mahojiano na wanahabari Sanga amekiri kuwa kamati tendaji haina mamlaka ya kumsimamisha katibu mkuu na jukumu hilo lipo chini ya mamlaka ya baraza la CWT Taifa kwa mujibu wa katiba ya CWT kifungu 22.2 hivyo katibu mkuu ataendelea na majukumu yake.