Hivi sasa kuna wagombea 12 katika chama cha Republican wanaotaka kugombania nafasi ya kukiwakilisha chama chao katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2024.
Wapinzani wengine kadhaa wamejitosa wiki hii katika kinyang’anyiro cha urais kwa chama cha Republican kujaribu kumzuia rais wa zamani Donald Trump kuchaguliwa kukiwakilisha chama katika uchaguzi wa rais kwa mara ya tatu mfululizo.
Miongoni mwao ni aliyekuwa Gavana wa jimbo la New Jersey, Chris Christie, mshirika wa Trump aliyegeuka kuwa mpinzani kwa mara nyingine tena. Gavana wa sasa, bilionea Doug Burgum wa North Dakota, pia amezindua kampeni yake.
Na siku ya Jumatano, Makamu Rais wa Trump aliyemtii wa muda mrefu, Mike Pence, alitangaza azma ya kipekee ya kushindana na mkuu wake wa zamani, ikiwa ni mara ya kwanza katika muda wa miaka 80 kufanyika hapa Marekani.
Pence hakupoteza muda kumkosa Trump kwa namna ambayo amekua akiepuka kufanya. Ninaamini kwamba yeyote anayejiweka juu ya Katiba kamwe asiwe rais wa Marekani, Pence alisema katika hotuba yake ya kwanza ya kampeni za urais siku ya Jumatano katika jimbo la Iowa. Aliongeza kusema kuwa, na yeyote anayemtaka mtu mwingine awe juu ya Katiba kamwe asiruhusiwe kuwa rais wa Marekani.
Hivi sasa kuna wagombea 12 katika chama cha Republican wanaotaka kugombania nafasi ya kukiwakilisha chama chao katika uchaguzi mkuu wa 2024.