UBAO wa Uwanja wa Uhuru unasoma Simba 3-1 Coastal Union ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Saido Ntibanzokiza alifunga bao la kuweka usawa dakika ya 13 akisawazisha bao la Coastal Union waliopachika bao la kuongoza kwa pigo la penalti dakika ya 7 kupitia kwa Amza Moboubarack.
John Bocco kipindi cha pili amepachika bao la pili kwa Simba dakika ya 56 na kamba ya tatu imepachikwa na Saido Ntibanzokiza anayefikisha mabao 17 kwenye ligi.
Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili ikiwa ni wa mwisho kwa timu zote ndani ya Bongo na mabingwa ni Yanga ambao wanamaliza na Tanzania Prisons ya Mbeya.