Mkoa wa Manyara umeongoza katika mchezo wa riadha kurusha Mkuki Wasichana na Wavulana katika mashindano ya UMITASHUMTA bada ya kuibuka washindi katika michezo iliyochezwa Ijumaa tarehe 09 Juni 2023 kwenye viwanja vya Shule ya Sekondri Wavulana Tabora.
Manyara iliongoza kwa upande wa Wavulana na wasichana baada ya wachezaji wake Kikwete Mabeo kurusha Mita 45.90 na Esta Motoja upande wa wasichana kurusha Mita 32.18
Nafasi ya pili Wavulana ilienda Mkoa Jirani wa Arusha baada ya Lukumok Lenuta kurusha mkuki umbali wa Mita 45.07, akifuatiwa na Jacksaon Denita wa Manyara aliyemaliza kwa Mita 41.03 huku Athuman John wa Mara akifikia Mita 35.45.
Mikoa mingine iliyofuata ni Kilimanjaro ambao washiriki wake wawili Emmanuel Msemle na Joseph Kitivo waliongozana kwenye nafasi ya 5 na 6 wakirusha Mita 35.09 na 23.83 wakifuatiwa na Shafii Hamis wa Dodoma Mita 33.10 na Shukuru Loya pia wa Dodoma Mita 33.04.
Upande wa wasichana nafasi ya pili ilienda tena kwa Manyara baada ya Jackli Ginyagha kurusha Mita 30.05 akifuatiwa na Veroica Marwa aliyeshika nafasi ya tatu kwa Mita 28.10 na nafasi ya nne kweda mkoai Kilimaajaro kwa Veroika Laizer Mita 25.18
Mikoa ya Taga, Sigida, Arusha na Tabora iliambulia afasi nne zilizosalia wakati fainali ikitarajiwa kufanyika Jumamosi na Jumapili ili kumpata Bingwa mchezo wa kushusha Mkuki katika mashindao ya umitashumta 2023.