UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa, kishindo kinakuja ndani ya Bongo kutokana na mipango inayoandaliwa kwenye usajili wa timu hiyo.
Simba imegotea nafasi ya pili ikiwa na pointi 73 kwenye ligi, huku ikishuhudia watani zao wa jadi Yanga wakisepa na taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 wakiwa na pointi 78.
Ikumbukwe kwamba, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, Simba imegotea hatua ya robo fainali baada ya kuondolewa na Wydad Casablanca.
Akizungumza Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema watakuja na kitu cha kipekee kwenye usajili jambo litakaloacha kishindo.
“Unaona tumeshindwa kufanya vizuri msimu huu, hilo lipo wazi, lakini tunakuja na kishindo kikubwa ambacho kitaturudisha kwenye ubora wetu hasa kwa kusajili wachezaji bora.
“Baada ya ligi kuisha, tunaanza kazi nyingine ya kuwaleta wachezaji bora na wenye uwezo wa kucheza ndani ya Simba unajua Simba ina wachezaji wake ambao wana hadhi ya kucheza mashindano makubwa,” alisema Ally.