Na Paul Kayanda
MCHIMBAJI mdogo wa Madini ya Almasi katika Mgodi wa Nyang’hwale uliopo Kijiji cha Nyambula Kata ya Ngogwa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, Bundala Makoye (53) mkazi wa Kata ya Busangi Halmashauri ya Msalala amefariki kwa kufukiwa na kifusi cha Udogo wakati akichimba madini hayo.
Akizungumza na Divine Fm Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambula Omary Mohamed amesema kuwa licha ya kupata taarifa kwa wananchi kuhusu tukio la mchimbaji huyo kufariki dunia wakati akichimba Madini ya Almasi lakini Kijiji hakina taarifa kuhusu vifo vinavyotokea kwenye Mgodi huo zaidi ya kusikia.
Hata hivyo Sebastian Nkwabi ni mmoja kati ya familia ya marehemu anadhibitisha kutokea kwa kifo cha ndugu yake huyo wakati akichimba madini hayo kwenye mgodi wa almasi Nyang’hwale na kwamba aliokolewa tayari akiwa katika hatua za mwisho kutokana na kupondwa jiwe na kupasuka mguu lakini baada ya kukimbizwa katika hospitali ya manispaa ya Kahama ndipo akaaga Dunia alipokuwa akipatiwa matibabu.
Hata hivyo mmoja kati ya viongozi wa mgodihuo, aliyejitambulisha kwa jina moja la William alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo kwa njia ya simu yake ya kiganjani haya hapa ni majibu yake.