Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema CCM ndiyo chama kinachofaa kuongoza Zanzibar.
Amewahimiza umoja na mshikamano kwa wanachama wa CCM kujiandaa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Ameyasema hayo tarehe 11 Juni 2023 ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa akizungumza na Viongozi wa CCM ngazi ya Shina, Wajumbe wa Halmashauri Jimbo, Wilaya na Mkoa huo.
Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi amewataka wana CCM kuvunja makundi, watakaoendeleza kuchukuliwa hatua na kamati za maadili za CCM .
Vilevile ametoa rai kufanyika kwa mafunzo ya itikadi kwa ngazi zote kwa Viongozi wa CCM pamoja na kuhimiza kuendelea kufanyika vikao vya kikatiba katika kila ngazi.